DKT. KIJAJI: USHINDI WA TUZO ZA UTALII DUNIANI NI MATUNDA YA FILAMU YA “TANZANIA: THE ROYAL TOUR”.
Na Philipo Hassan – Dodoma Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameeleza kuwa Tanzania kuibuka mshindi wa Tuzo mbalimbali za utalii duniani ni matunda ya filamu ya “Tanzania: The Royal Tour” iliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri Dkt. Kijaji amesema hayo leo Desemba 15, 2025 katika hafla ya kupokea na kusherehekea tuzo za kimataifa ambazo Tanzania imeshinda katika sekta ya utalii kwa mwaka 2025. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Mtumba Jijini Dodoma. “Tunautambua na kuuthamini kwa upekee mchango wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Filamu ya “Tanzania: The Royal Tour”. Hakika mafanikio haya ni jitihada zake mahsusi kwa yeye binafsi kufungua milango ya kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa, ambapo leo hii tunashuhudia jumla ya tuzo 5 za utalii ambapo zimeendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania duniani” ~ alieleza Dkt. Kijaji. Dkt. Kijaji aliongeza kuwa “Tanzania kuteuliwa...